An-Nahl
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
مَن كَفَرَ بِٱللَّهِ مِنۢ بَعْدِ إِيمَـٰنِهِۦٓ إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُۥ مُطْمَئِنٌّۢ بِٱلْإِيمَـٰنِ وَلَـٰكِن مَّن شَرَحَ بِٱلْكُفْرِ صَدْرًا فَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ مِّنَ ٱللَّهِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ۱۰۶ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ ٱسْتَحَبُّوا۟ ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا عَلَى ٱلْـَٔاخِرَةِ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلْكَـٰفِرِينَ ۱۰۷ أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ طَبَعَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَسَمْعِهِمْ وَأَبْصَـٰرِهِمْ ۖ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْغَـٰفِلُونَ ۱۰۸
{106 - 108} Yeye mukufu anajulisha juu ya hali mbaya ya wale waliomkufuru baada ya kumuamini, kwa hivyo akapofuka baada ya kwamba alikuwa ana uwezi wa kuona, na akarudi katika upotofu baada ya kwamba alikuwa ameongoka, na akakifungulia kifua chake ukafiri, na akauridhia, na akatulia nao, basi wana ghadhabu kubwa kutoka kwa Mola wao Mlezi, Mwingi wa kurehemu, ambaye anapokasirika, hakuna chochote kinachoweza kuizuia ghadhabu yake, na tena kila kitu kinawakasirikia hao. "Na wao wana adhabu kubwa" yenye kudumu milele. Na hilo ni kwa kuwa wao "wameupendelea uhai wa dunia hii kuliko Akhera" ambapo ya kwamba walirudi nyuma kwa visigino vyao kwa sababu ya tamaa ya kupata kitu katika vitu vya kidunia visivyokuwa na thamani, na kuitaka sana, na kuipa mgongo heri ya Akhera. Na walipochagua ukafiri badala ya imani, Mwenyezi Mungu akawazuia uongofu, kwa hivyo hakuwaongoa. Hili ni kwa sababu ukafiri ndio sifa yao, basi na Mwenyezi Mungu akafunga nyoyo zao, kwa hivyo heri yoyote haiwezi kuingia humo. Na pia akafunga masikio yao na macho yao, kwa hivyo hakipiti humo chochote cha kuwafaidi na kufikia nyoyo zao. Basi wakaenewa na kughafilika, na wakazungukwa na kuangushwa, na wakanyimwa rehema za Mwenyezi Mungu ambazo zimeenea kila kitu. Na hayo ni kwa sababu rehema zake ziliwajia, lakini wakazikataa, na zikaekwa mbele yao, lakini hawakuzikubali.