Al-Hijr
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
لَا تَمُدَّنَّ عَيْنَيْكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعْنَا بِهِۦٓ أَزْوَٰجًا مِّنْهُمْ وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَٱخْفِضْ جَنَاحَكَ لِلْمُؤْمِنِينَ ۸۸
{88} Na kama Mwenyezi Mungu alimpa Qur'ani tukufu pamoja na saba hizo, basi alimpa kilicho bora zaidi wanachokishindania washindani na kikubwa zaidi wanachokifurahia Waumini. "Sema: Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake! Basi na wafurahi kwa hayo. Haya ni bora kuliko hayo wanayoyakusanya." Na ndiyo maana akasema baada yake, "Kamwe usivinyoshee macho yako vitu tulivyowastarehesha kwavyo makundi fulani kati yao." Yaani, usipendezwe kupendezwa ambako kutakufanya kuishughulisha fikira yako na matamanio ya dunia ambayo wanastarehe kwayo, na wajinga wamedanganyika kwayo. Na tosheka na yale aliyokupa Mwenyezi Mungu miongoni mwa yale yanayorudiwarudiwa na Qur-ani Tukufu. "Wala usiwahuzunikie," kwa kuwa hakuna heri yoyote inayotarajiwa kwao, wala hakuna manufaa yanayongojewa. Nawe una kibadala kizuri zaidi miongoni mwa waumini kuliko wao. "Na wainamishie bawa lako (la huruma) Waumini." Yaani, walainishie ubawa wako na waonyeshe tabia nzuri kwa kuwapenda, kuwakirimu, na kuwapenda.