Hud
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
قَالُوا۟ يَـٰهُودُ مَا جِئْتَنَا بِبَيِّنَةٍ وَمَا نَحْنُ بِتَارِكِىٓ ءَالِهَتِنَا عَن قَوْلِكَ وَمَا نَحْنُ لَكَ بِمُؤْمِنِينَ ۵۳
{53} Wakasema wakiikataa kauli yake: {Ewe Hud! Hujatuletea ushahidi ulio wazi." Ikiwa makusudio yao ni ushahdii ulio wazi wanaoupendekeza wao, basi hili si jambo la lazima ili ayasemayo yawe ndiyo haki. Bali la lazima ni kwamba nabii aje na ishara inayoashiria usahihi wa kile alichokuja nacho. Na kama makusudio yao ni kwamba hakuwajia na ushahidi unaoshuhudia usahihi wa kile alichokuja nacho, basi hakika walidanganya katika hilo. Kwa maana, hakuwahi kuja nabii yeyote kwa kaumu yake isipokuwa Mwenyezi Mungu alituma kwa mikono yake Ishara ambazo wanaadamu wanaamini mfano wake, na kama hangekuwa na ishara isipokuwa kuwalingania tu wampwekeshee Mwenyezi Mungu Dini bila ya mshirika yeyote, na kuamrisha kila tendo jema, na tabia nzuri, na kukataza kila tabia mbaya miongoni mwa kumshirikisha Mwenyezi Mungu na dhuluma na aina mbalimbali za maovu, pamoja na yale anayosifika kwayo Hud, amani iwe juu yake ya sifa ambazo haziwi isipokuwa viumbe bora zaidi na wakweli wao zaidi. Basi Haya yangetosha kuwa ishara na ushahidi juu ya ukweli wake. Bali watu wenye akili na ufahamu wanaona kwamba ishara hii ni kubwa zaidi kuliko mambo ya kimuujiza ambayo baadhi ya watu wanayaona kuwa ndiyo miujiza tu. Na miongoni mwa ishara zake na ushahidi wake ulio wazi unaoashiria ukweli wake ni kwamba alikuwa mtu mmoja tu bila ya wa kumnusuru wala wasaidizi, lakini yeye akawa anasema kwa sauti kubwa katika kaumu yake na kuwaita na kuwaona kwamba hawana uwezo. Na anawaambia: Hakika mimi ninamtegemea Mwenyezi Mungu wangu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. "Hakika, mimi ninamshuhudisha Mwenyezi Mungu, na nyinyi shuhudieni, ya kwamba mimi niko mbali na hao mnaowafanya washirika. Badala ya Yeye. Basi nyinyi nyote nipangieni njama, na kisha msinipe muhula!" Ilhali wao ni maadui ambao wana uwezo na ushindi, na wanataka kuzima nuru aliyo nayo kwa njia yoyote ile, naye akawa hashughuliki nao wala kuwajali, nao wakawa wameshindwa na hawawezi kumfikishia mabaya yoyote. hakika katika hayo zimo ishara kwa kaumu wanaotumia akili. Na kauli yao: "Wala sisi hatuiachi miungu yetu kwa kufuata kauli yako." Yaani, hatuachi kuabudu miungu yetu kwa sababu tu ya yale uliyoyasema, ambayo hukuyasimamishia ushahidi wowote - kulingana na madai yao. "Na wala sisi hatukuamini wewe" na huku ni kumkatisha kwao tamaa nabii wao Hud - amani iwe juu yake - katika kuamini kwao. Na kwamba hawataacha kuendelea kutangatanga kiupofu katika ukafiri wao.