Yunus
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
أَلَآ إِنَّ لِلَّهِ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَن فِى ٱلْأَرْضِ ۗ وَمَا يَتَّبِعُ ٱلَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ شُرَكَآءَ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ ۶۶
{66} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba Yeye ni vyake vilivyo katika mbingu na ardhi, kwa kuviumba, na kuvimiliki [navyo ni waja wake] ambavyo anaviendesha anavyotaka kwa hukumu zake. Kwani hivyo, vyote vinamilikiwa na Mwenyezi Mungu, vimetiishwa na vinaendeshwa, wala havistahiki chochote katika ibada wala si washirika wa Mwenyezi Mungu kwa namna yoyote ile. Na kwa sababu ya hili ndiyo akasema, "Na wala hawawafuati washirika wowote hao wanaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu. Wao hawafuati isipokuwa dhana tu" ambayo haisaidii chochote mbele ya haki; "na hawasemi isipokuwa uongo " katika hilo. Nalo ni uongo na masingizio. Kwa hivyo, ikiwa ni wakweli kwamba hao ni washirika wa Mwenyezi Mungu, basi na wadhihirishe sifa wanazostahiki kwazo uzito wa chembe katika ibada; lakini hawataweza. Basi Je, yuko yeyote miongoni mwao anayeumba chochote, au anayeruzuku, au anayemiliki chochote katika viumbe, au anayeendesha usiku na mchana ambao Mwenyezi Mungu aliufanya kuwa nguzo ya maisha ya mwanadamu?