Yunus
این ترجمهٔ تفسیر سعدی است، همانگونه که IslamHouse.com آن را در saadi.islamenc.com منتشر میکند و از صفحههای آن سایت گرفته شده است. سایت نمیگوید چه کسی آن را ترجمه کرده و از کدام چاپ پیروی میکند، و برای برداشتن متن آن شرطی بیان نمیکند، پس حق نمایش آن تأیید نشده است. کسی آن را با کتاب چاپی مقایسه نکرده و عالمی آن را بررسی نکرده است. هر بخش در کنار آیههایی آمده که دربارهٔ آنها توضیح میدهد و این آیهها متن قرآن از Tanzil است، همانگونه که آنجا هست؛ آیهای که سایت توضیح جداگانهای برایش نمیدهد با بخش پیش از خود میآید، و فهرست هر چنین آیهای را نام میبرد. سبیل چیزی از آن را ننوشته و ترجمه نکرده است.
متن ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)برداشتهشده در 2026-10-22
قُل لَّوْ شَآءَ ٱللَّهُ مَا تَلَوْتُهُۥ عَلَيْكُمْ وَلَآ أَدْرَىٰكُم بِهِۦ ۖ فَقَدْ لَبِثْتُ فِيكُمْ عُمُرًا مِّن قَبْلِهِۦٓ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ۱۶
{16} { Sema, “Mwenyezi Mungu angelitaka, nisingeliwasomea, wala nisingelikuwa mwenye kukijua zaidi yenu. Kwani nalikwisha kaa miongoni mwenu umri mzima” mrefu “kabla yake!” Yaani, kabla ya kuisoma na kabla ya nyinyi na mimi kuijua, wala haikunijia kwenye akili wala haikuingia katika fikira zangu. "Kwani, hamtii akilini?” Kwamba kuwa sikuitunga katika muda wa maisha yangu, wala hakikutokea kwangu chochote kinachoonyesha hivyo; basi nitaitunga baada ya hapo ilhali nimekaa miongoni mwenu muda mrefu, huku mnajua uhakika wa hali yangu kwamba mimi sijui kusoma na kuandika, wala sisomi, wala sijifunzi kutoka kwa yeyote. Kisha nikawajia na kitabu kikuu ambacho kiliwashinda wenye ufasaha na kikawapiku wanachuoni. Basi je, inawezekana baada ya hayo kwamba kiwe nimekitunga tu mimi mwenyewe? Au huu ni ushahidi wa uhakika kwamba ni uteremsho kutoka kwa Mwenye hekima, Msifiwa? Na ikiwa mtatumia akili na fikira zenu, na akili zenu, na mkaitafakari hali yangu na hali ya kitabu hiki, basi mngekuwa na uhakika usiokubali shaka yoyote kwamba ni cha ukweli, na kwamba ndiyo haki ambayo baada yake hakuna isipokuwa upotofu. Lakini ikiwa mtakataa isipokuwa kukadhibisha na ukaidi, basi nyinyi hakuna shaka ni madhalimu.