Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tawba
Sūrah 9

At-Tawba

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 83

فَإِن رَّجَعَكَ ٱللَّهُ إِلَىٰ طَآئِفَةٍ مِّنْهُمْ فَٱسْتَـْٔذَنُوكَ لِلْخُرُوجِ فَقُل لَّن تَخْرُجُوا۟ مَعِىَ أَبَدًا وَلَن تُقَـٰتِلُوا۟ مَعِىَ عَدُوًّا ۖ إِنَّكُمْ رَضِيتُم بِٱلْقُعُودِ أَوَّلَ مَرَّةٍ فَٱقْعُدُوا۟ مَعَ ٱلْخَـٰلِفِينَ 83

{83} "Basi Mwenyezi Mungu akikurudisha kwenye kikundi kimoja miongoni mwao" nao ni wale waliosalia nyuma bila ya udhuru, wala hawakuhuzunika juu ya kusalia kwao nyuma "na wakakutaka idhini ya kutoka" katika visivyokuwa vita hivi watakapoona wepesi. "Basi sema" uwaambie kama adhabu kwao "Nyinyi hamtatoka pamoja nami kabisa, wala hamtapigana na adui pamoja nami," kwa maana Mwenyezi Mungu atatosheleza bila nyinyi. "Hakika nyinyi mliridhia kukaa nyuma mara ya kwanza, basi kaeni pamoja na hao waliobakia nyuma." Na haya ni kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Na tutazigeuza nyoyo zao na macho yao kama vile hawakuiamini mara ya kwanza." Kwa maana Mwenye kujitia uzito anayesalia nyuma ya yale yaliyoamrishwa wakati wa kuwepo fursa, hatawezeshwa juu yake baada ya hapo, na itazuiliwa kati yake na hilo. Na ndani yake pia kuna kuwapa nguvu, kwa maana inapothibiti kwa Waislamu kwamba hawa ni katika wale waliozuiwa kutoka kwenda katika jihadi kwa sababu ya maasia yao, linakuwa hilo ni kemeo kwao, na fedheha kwao, na adhabu ili asifanye yeyote kama waliyoyafanya.