At-Tawba
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
إِلَّا تَنفِرُوا۟ يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًا وَيَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْـًٔا ۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ 39
{39} Kisha akaahidi adhabu ikiwa hawatoki kwenda katika vita, kwa hivyo akasema: "Kama hamuendi, atawaadhibu adhabu chungu" katika dunia na Akhera. Kwani kutotoka wakati wa hali ya kuitwa kutoka ni miongoni mwa madhambi makubwa ambayo yanasababisha adhabu kali zaidi, Kwa sababu ya madhara makubwa yaliyo ndani yake. kwa maana mwenye kubakia nyuma amemuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akafanya makatazo yake, na hakusaidia katika kuinusuru Dini ya Mwenyezi Mungu, wala hakukitetea Kitabu cha Mwenyezi Mungu na sheria yake, wala hakuwasaidia ndugu zake Waislamu dhidi ya adui yao ambaye anataka kuwaangamiza na kuifutilia mbali dini yao, na huenda akamuiga asiyekuwa yeye miongoni mwa madhaifu wa imani; bali pengine akawadhoofisha wale wanaopigana jihadi dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu. Basi anastahili yule ambaye hali yake ni hii kwamba Mwenyezi Mungu amuahidi ahadi ya adhabu kali, ndiyo akasema, "Kama hamuendi, atawaadhibu adhabu chungu, na atawabadilisha na kaumu wasiokuwa nyinyi" nao hawatakuwa mfano wenu. "Wala nyinyi hamtamdhuru chochote" kwani Yeye Mtukufu alichukua jukumu la kuinusuru dini yake na kuliinua neno lake; basi ni sawa ikiwa mtatekeleza amri ya Mwenyezi Mungu au muitupe nyuma yenu kwenye migongo. "Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu." Hakimshindi kitu chochote anachotaka, wala hakuna yeyote wa kumshinda.