Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Maaida
Sūrah 5

Al-Maaida

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 52

فَتَرَى ٱلَّذِينَ فِى قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يُسَـٰرِعُونَ فِيهِمْ يَقُولُونَ نَخْشَىٰٓ أَن تُصِيبَنَا دَآئِرَةٌ ۚ فَعَسَى ٱللَّهُ أَن يَأْتِىَ بِٱلْفَتْحِ أَوْ أَمْرٍ مِّنْ عِندِهِۦ فَيُصْبِحُوا۟ عَلَىٰ مَآ أَسَرُّوا۟ فِىٓ أَنفُسِهِمْ نَـٰدِمِينَ 52

{52} Na Mwenyezi Mungu alipowakataza Waumini kuwafanya wao kuwa marafiki wadani, akajulisha kwamba miongoni mwa wale wanaodai kuwa na imani kuna kundi fulani linalowafanya kuwa marafiki wandani. Kwa hivyo akasema, "Basi, utawaona wale wenye maradhi katika nyoyo zao," yaani, shaka na unafiki na udhaifu wa imani, husema: hakika kuwafanya kwetu wao kuwa marafiki wandani ni kwa sababu ya haja. Kwani sisi hakika "tunahofu kusibiwa na mabadiliko." Yaani, mabadiliko mazuri yawajie Mayahudi na Wakristo; na ikiwa mabadiliko mazuri yatakuwa upande wao, basi tayari tutakuwa na mkono kwao ambao watatulipa kwa sababu yake. Na hii ni dhana yao mbaya juu ya Uislamu. Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema akiwakanusha katika dhana yao mbaya; "Basi huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi," ambao kwa huo Mwenyezi Mungu ataufanya Uislamu kuwa na nguvu zaidi juu ya Mayahudi na Wakristo, na Waislamu wawashinde. "Au jambo jingine kutoka kwake, ambalo wanafiki watakata tamaa kwa sababu yake katika ushindi wa makafiri miongoni mwa Mayahudi na wengineo. "Na wakawa kwa yale waliyoyaficha katika nafsi zao ni wenye kujuta," kwa yale waliyofanya, na yakawadhuru bila ya manufaa yoyote waliyoyapata. Kisha ukaja ule ushindi ambao Mwenyezi Mungu aliwanusuru kwao Uislamu na Waislamu, na akaudhalilisha kwao ukafiri na makafiri. Kwa hivyo wakajuta na kupata huzuni ambayo Mwenyezi Mungu tu ndiye anayejua vyema.