An-Nisaa
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
ٱللَّهُ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۗ وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ ٱللَّهِ حَدِيثًا 87
{87} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu upekee wake katika Umoja, na kwamba hakuna muabudiwa wala mungu isipokuwa Yeye kwa sababu ya ukamilifu wake katika dhati yake na sifa zake. Na kwa kuwa Yeye ndiye wa pekee katika uumbaji, na uendeshaji mambo, na neema za dhahiri na ndani. Na hilo linalazimu kuamrisha kwamba kuabudiwa na kujikurubisha Kwake kupitia aina zote za kumfanyia ibada; kwa sababu Yeye peke yake ndiye anayestahiki hayo, na ndiye atakayewalipa waja wake kwa yale waliyoyatenda miongoni mwa ibada zake au waliyoyaacha katika hayo. Na ndio maana akaapa juu ya kupatikana kwa pahali pa malipo, ambapo ni Siku ya Qiyama, akasema: "Kwa yakini, atawakusanya;" yani: wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu katika pahali pamoja, katika "Siku ya Qiyama. Halina shaka hilo." Yani hakuna shaka wala mchanganyiko kwa njia yoyote ile kwa ushahidi wa kiakili na ushahidi wa kusikia. Basi, ushahidi wa kiakili ni ule tunaouona wa kuihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na kuwepo kwa uumbaji wa kwanza, ambao kutokea kwa kule kwa pili kuna uwezekano mkubwa zaidi kutokea kuuliko (kwa kwanza). Na katika hekima ambazo inathibitisha kimadhubuti kuwa Mwenyezi Mungu hakuumba viumbe wake bure tu ni kwamba wanakuwa hai, kisha wanakufa. Na ama ushahidi wa kusikiwa, ni kule kujulisha kwa aliye Mkweli zaidi miongoni mwa wakweli juu ya hilo, na hata kuapa kwake kwayo. Na ndiyo maana akasema, “Na ni nani msema kweli kuliko Mwenyezi Mungu?” Kadhalika alimwamrisha Mtume wake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kwamba aape kwalo katika sehemu zaidi ya moja katika Qur-ani. Kama vile kauli yake, “Wale waliokufuru walidai kuwa hawatafufuliwa. Sema: Sivyo hivyo? Ninaapa kwa Mola wangu Mlezi! Hapana shaka mtafufuliwa, kisha hapana shaka mtaambiwa yale mliyoyatenda. Na hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.” Na katika kauli yake, “Na ni nani mkweli zaidi katika mazungumzo kuliko Mwenyezi Mungu.” “Na ni nani mkweli zaidi kwa kauli kuliko Mwenyezi Mungu.” Kuna kujulisha kwamba mazungumzo yake, na kujulisha kwake, na kauli zake yako katika daraja za juu kabisa za ukweli. Bali ndiyo ya juu yake zaidi. Kwa maana, kila kilichosemwa kuhusu imani, na elimu, na matendo katika yale yanayopingana na yale ambayo Mwenyezi Mungu alijulisha, basi hayo batili kwa sababu ya kupingana kwake na habari za kweli yenye yakini. Basi, hayawezi kuwa kweli.