Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
Sūrah 4

An-Nisaa

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 20

وَإِنْ أَرَدتُّمُ ٱسْتِبْدَالَ زَوْجٍ مَّكَانَ زَوْجٍ وَءَاتَيْتُمْ إِحْدَىٰهُنَّ قِنطَارًا فَلَا تَأْخُذُوا۟ مِنْهُ شَيْـًٔا ۚ أَتَأْخُذُونَهُۥ بُهْتَـٰنًا وَإِثْمًا مُّبِينًا 20

{20} Na haya yote ni pamoja na uwezekano wa kumshikilia na kutokuwepo kwa kilichokatazwa. Na ikiwa ni lazima kutengana na hakuna nafasi ya kumshikilia; basi kumshikilia si lazima. Bali pindi, "mkitaka kubadilisha mke pahali pa mke," yani, kumtaliki mke mmoja na kumuoa mwingine, basi hakuna dhambi juu yenu katika hayo, wala hakuna ubaya. Lakini ikiwa "mmempa mmoja wao," yani yule aliyeachwa au yule aliyemuoa "mali nyingi; basi msichukue katika hiyo kitu chochote." Bali wapeni kwa wingi wala msiwacheleweshe. Na katika Aya hii kuna ushahidi kwamba mahari nyingi haijaharamishwa, pamoja na kwamba lililo bora zaidi na lifaalo ni kufuata mfano wa Mtume Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - katika kupunguza mahari. Na namna ya ushahidi wenyewe ni kwamba Mwenyezi Mungu alijulisha kuhusu jambo lililotokea kutoka kwao, na wala hakuwakataza. Kwa hivyo, hilo likaashiria kutoharamishwa kwake. Hata hivyo, inaweza kukatazwa kupeana mahari nyingi ikiwa hilo linajumuisha uharibifu wa kidini na kutokuwepo masilahi yanayopingwa. Kisha akasema, "Je, mtachukua kwa dhulma na kosa lilio wazi?" Kwani hili haliruhusiki, hata mkidanganya juu yake kwa kila aina ya hila. Kwani kosa lake liko wazi.