An-Nisaa
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ بِٱللَّهِ وَٱعْتَصَمُوا۟ بِهِۦ فَسَيُدْخِلُهُمْ فِى رَحْمَةٍ مِّنْهُ وَفَضْلٍ وَيَهْدِيهِمْ إِلَيْهِ صِرَٰطًا مُّسْتَقِيمًا 175
{175} Lakini watu waligawanyika kulingana na kuiamini Qur-ani na kunufaika nayo sehemu mbili: "Ama wale waliomuamini Mwenyezi Mungu," yaani, walikiri kuwepo Kwake, na kusifika kwake na kila sifa kamili, na kutakasika kwake na kila upungufu na kasoro. "Na wakashikamana naye," yaani, walikimbilia kwa Mwenyezi Mungu, na wakamtegemea, na wakajiweka mbali na hila zao na uwezo wao, na wakaomba msaada kwa Mola wao Mlezi. "Basi atawaingiza katika rehema itokayo kwake, na fadhila." Yaani atawafunika kwa rehema maalum, na awawezeshe mema, na awalipe malipo mengi, na awaepushe na balaa na machukizo. "Na atawaongoa kwenye Njia iliyonyooka." Yaani, awawezeshe kufikia elimu na matendo,kuijua haki na kuifanyia kazi. Yaani, na mwenye kutomwamini Mwenyezi Mungu, na kushikamana naye, na kushikamana na Kitabu chake, atawazuia rehema yake, na atawaharamishia fadhila yake, na awaachie nafsi zao, kwa hivyo hawakuongoka. Bali walipotea upotovu ulio wazi; kama adhabu kwao kwa sababu ya kuacha kwao imani, basi wakaambulia patupu na kunyimwa. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu msamaha, na afia, na salama.