Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
Sūrah 4

An-Nisaa

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 147

مَّا يَفْعَلُ ٱللَّهُ بِعَذَابِكُمْ إِن شَكَرْتُمْ وَءَامَنتُمْ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ شَاكِرًا عَلِيمًا 147

{147} Kisha Yeye Mtukufu akajulisha kuhusu ukamilifu wa kutohitaji kwake, na upana wa ustahimilivu wake, na rehema yake, na wema wake. Akasema, "Mwenyezi Mungu atafanyia nini kuwaadhibu ikiwa mtashukuru na mkaamini?" Na hali ni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushukuru, Mwenye kujua. Anawapa wanaovumilia mizigo kwa ajili yake, wenye kudumu katika matendo, ni Mwingi wa malipo na mkunjufu wa wema. Na mwenye kuacha kitu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atampa kilicho bora zaidi kuliko hicho. Na pamoja na haya, anajua dhahiri zenu na ndani yenu, na matendo yenu, na yale yanayotoka kwake (mja) ya kumkusudia Yeye tu na ukweli na kinyume cha hayo. Naye anataka toba kutoka kwenu, na kumnyenyekea, na kurudi kwake. Na mkirudi kwake, basi atafanyia nini kuwaadhabu? Kwani, yeye haponi kwa kuwaadhibu, wala hafaidiki na kuwatesa. Bali muasi hajidhuru isipokuwa mwenyewe, kama vile matendo ya mwenye kutii ni kwa ajili yake mwenyewe. Na shukrani ni kunyenyekea kwa moyo, na kukiri kwake neema ya Mwenyezi Mungu, na kusifu kwa ulimi yule anayeshukuriwa, na matendo ya viungo katika kumtii Yeye, na kwamba asijisaidie na neema yake katika kumuasi.