An-Nisaa
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
وَمَن يَكْسِبْ خَطِيٓـَٔةً أَوْ إِثْمًا ثُمَّ يَرْمِ بِهِۦ بَرِيٓـًٔا فَقَدِ ٱحْتَمَلَ بُهْتَـٰنًا وَإِثْمًا مُّبِينًا 112
{112} Kisha akasema: "Na mwenye kuchuma kosa," yani dhambi kubwa, “au dhambi” yani kilicho chini ya hilo. “Kisha akamsingizia,” yani akamtuhumu kwa dhambi yake hiyo "asiye na hatia” ya dhambi hiyo hata kama ana dhambi. “Basi amejitwika masingizio na dhambi iliyo wazi.” Yani hakika amebeba kwenye mgongo wake masingizio kwa asiyekuwa na hatia, na dhambi iliyo dhahiri, iliyo wazi. Na hili linaashiria kuwa hili ni katika madhambi makubwa na yenye kuangamiza. Kwani limechanganya maovu kadhaa: kuchuma kosa kubwa, na dhambi, kisha kumtuhumu yule ambaye hakuifanya kwamba ameifanya. Kisha uongo mbaya kwa kujiondoa na kumtuhumu asiyekuwa na hatia, kisha yale yanayotokana na hayo ya adhabu ya kidunia inayozuilika kwa yule ambaye imewajibika juu yake, na kusimamishwa juu ya yule ambaye haistahiki. Kisha yale yanayotokana na hayo pia ya watu kuzungumza kuhusu huyo asiyekuwa na hatia na mengineyo miongoni mwa maovu ambayo tunamwomba Mwenyezi Mungu atupe salama kutokana nayo na kutokana na kila maovu.