Az-Zumar
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
وَإِذَا مَسَّ ٱلْإِنسَـٰنَ ضُرٌّ دَعَا رَبَّهُۥ مُنِيبًا إِلَيْهِ ثُمَّ إِذَا خَوَّلَهُۥ نِعْمَةً مِّنْهُ نَسِىَ مَا كَانَ يَدْعُوٓا۟ إِلَيْهِ مِن قَبْلُ وَجَعَلَ لِلَّهِ أَندَادًا لِّيُضِلَّ عَن سَبِيلِهِۦ ۚ قُلْ تَمَتَّعْ بِكُفْرِكَ قَلِيلًا ۖ إِنَّكَ مِنْ أَصْحَـٰبِ ٱلنَّارِ 8
{8} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya ukarimu wake kwa mja wake, ihsani yake, wema wake na uchache wa shukrani ya mja wake. Na kwamba wakati madhara yanampata kama vile ugonjwa, umaskini, au kuingia katika dhiki ya baharini au kwingineko, anajua kwamba hakuna awezaye kumwokoa katika hali hii isipokuwa Mwenyezi Mungu tu. Kwa hivyo anamuomba kwa unyenyekevu na kutubia kwake. Na anamuomba msaada katika kuondoa hayo yaliyompata, na anasisitiza kufanya hivyo. "Kisha" Mwenyezi Mungu "akimpa neema kutoka kwake" kwa kumuondoshea madhara na dhiki iliyokuwa imemsibu, "husahau yale aliyokuwa akimwomba zamani" na akawa ni kana kwamba hakupatwa na madhara yoyote, na akaendelea na ushirikina wake. "Na akamfanyia Mwenyezi Mungu washirika ili apoteze watu katika njia yake" na ajipoteze yeye mwenyewe. "Sema" ukimwambia huyu mkaidi aliyebadilisha neema ya Mwenyezi Mungu kwa kufuru: "Starehe na ukafiri wako ni kwa muda mchache, kwani hakika wewe utakuwa miongoni mwa watu wa Motoni." Hicho unachostarehe kwacho hakitakusaidia kitu ikiwa utaishia Motoni. "Waonaje kama tukiwastarehesha kwa miaka, kisha yakawafikia waliyokuwa wakiahidiwa. Yatawafaa nini yale waliyostareheshewa?"