Az-Zumar
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
وَسِيقَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ إِلَىٰ جَهَنَّمَ زُمَرًا ۖ حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءُوهَا فُتِحَتْ أَبْوَٰبُهَا وَقَالَ لَهُمْ خَزَنَتُهَآ أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ يَتْلُونَ عَلَيْكُمْ ءَايَـٰتِ رَبِّكُمْ وَيُنذِرُونَكُمْ لِقَآءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا ۚ قَالُوا۟ بَلَىٰ وَلَـٰكِنْ حَقَّتْ كَلِمَةُ ٱلْعَذَابِ عَلَى ٱلْكَـٰفِرِينَ 71
{71} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kwamba atahukumu kati waja wake aliowakutanisha katika uumbaji wake, riziki yake, usimamizi wake na katika mkusanyiko wao mahali ambapo viumbe watasimama Siku ya Kiyama, Mwenyezi Mungu Mtukufu akawatenganisha katika malipo yao, kama walivyotengana dunia kwa imani, ukafiri, uchamungu na uovu wao. Akasema: "Na wale waliokufuru wataongozwa kuiendea Jahannamu" huku wakipigwa mijeledi michungu na Malaika wakali hadi kwenye jela mbaya zaidi na sehemu ya kutisha sana, ambayo ni Jahannamu, ambayo imekusanya kila adhabu, taabu na haina raha yoyote. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Siku watakaposukumwa kwenye Moto kwa msukumo wa nguvu" kwa watakuwa wamekataa kuingia humo, kwa hivyo wataswagwa kwenda humo "kwa makundi" Kila kundi litaingia na kundi linalofanana nalo katika matendo yake na juhudi zake. Hapo watalaaniana wao kwa wao na watatengana wao kwa wao, "mpaka watakapoifikia itafunguliwa milango yake" watakapoifikia "na walinzi wake watawaambia" wakiwabashiria taabu na adhabu ya milele na yao wakiwakaripia kwa sababu walifanya matendo yaliyowafikisha mahali hapa pabaya "Kwani hawakukujilieni Mitume miongoni mwenu" mliowajua na mkajua ukweli wao na mkaweza kujifunza kutoka kwao "wakikusomeeni Aya za Mola wenu Mlezi" ambazo Mwenyezi Mungu aliwatuma nazo, zikibainisha haki ya yakini kwa hoja zilizo wazi zaidi, "na kukuonyeni mkutano wa siku yenu hii?" Yaani, haya yaliwalazimu nyinyi kuwafuata na kujihadhari na adhabu ya siku hii kwa kumcha Mungu. Lakini hali yenu ilikuwa tofauti na hali hii. "Watasema" wakikiri dhambi zao na kwamba hoja ya Mwenyezi Mungu ilithibiti juu yao. "Kwani!" Mitume wa Mola wetu Mlezi walitujia na Ishara zake na hoja zake zilizo wazi, na wakatubainishia kubainisha kukubwa zaidi, na wakatutahadharisha kutokana na siku hii. "Lakini limekwishathibiti neno la adhabu juu ya makafiri." Nalo litathibiti kwa kila aliyezikufuru Aya za Mwenyezi Mungu na akakapinga yale waliyoyaleta Mitume. Basi wakakiri dhambi zao na ikathibitika hoja juu yao.