Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sūrah 2

Al-Baqara

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 93

وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَـٰقَكُمْ وَرَفَعْنَا فَوْقَكُمُ ٱلطُّورَ خُذُوا۟ مَآ ءَاتَيْنَـٰكُم بِقُوَّةٍ وَٱسْمَعُوا۟ ۖ قَالُوا۟ سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا وَأُشْرِبُوا۟ فِى قُلُوبِهِمُ ٱلْعِجْلَ بِكُفْرِهِمْ ۚ قُلْ بِئْسَمَا يَأْمُرُكُم بِهِۦٓ إِيمَـٰنُكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ 93

(93) "Na tulipochukua ahadi yenu na tukauinua mlima juu yenu (tukakwambieni): Kamateni kwa nguvu haya tuliyokupeni na sikieni." yani kusikia kwa kukubali, kutii, na kuitikia. "Wakasema: Tumesikia na tumekataa!" Yani ikawa hii ndiyo hali yao. "Na wakanyweshwa nyoyoni mwao (imani ya kumwabudu) ndama." Yani wakapakwa ndani ya nyoyo zao kupenda ndama, na kupenda kumuabudu. Na huko kunyweshwa kwao ni kwa sababu ya kukufuru kwao. "Sema: Ni uovu mno iliyokuamrisheni imani yenu ikiwa ni wenye kuamini". Yani nyinyi mnadai kuwa mnaamini na mnajisifu kuwa mna dini ya haki. Hali ya kuwa nyinyi mliwauwa Manabii wa Mwenyezi Mungu na mkamchukua ndama kuwa mungu badala ya Mwenyezi Mungu; wakati Musa Nabii wa Mwenyezi Mungu alipokwenda mbali na nyinyi. Na hamkuyakubali maamrisho yake na makatazo yake isipokuwa baada ya vitisho na kuinua mlima juu yenu. Basi mkashikamana na kauli, na mkavunja hilo kwa matendo yenu. Basi imani gani hii mliyodai? Na hii ni dini gani? Na ikiwa hii ni imani kama mnavyodai, basi ni mbaya mno. Imani inayomwita anayeiamini katika upotovu na kuwakufuru Mitume wa Mwenyezi Mungu na kuasi kwa wingi. Na ilikwisha julikana kuwa imani sahihi inamuamrisha mwenyewe (mwenye imani) kila jema na inamkataza kila ovu. Kwa hivyo, ikabainika kwa hilo uongo wao na mgongano wao.