Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sūrah 2

Al-Baqara

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 78

وَمِنْهُمْ أُمِّيُّونَ لَا يَعْلَمُونَ ٱلْكِتَـٰبَ إِلَّآ أَمَانِىَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَظُنُّونَ 78

(78) "Na wamo miongoni mwao" yani miongoni hawa watu wa Kitabu "wasiojua kusoma" yani watu wa kawaida wasiokuwa miongoni mwa wenye elimu. "Hawakijui Kitabu isipokuwa uongo wanaoutamani," yani wao hawana fungu katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu isipokuwa kusoma tu. Na hawana habari kwa yale waliyokuwa nayo watu wa mwanzo ambao wanazijua hali zao haki ya kuzijua. Na hawa (watu) wana dhana tu, na mila za watu wa elimu miongoni mwao. Basi akawataja katika hizi Aya wanachuoni wao, watu wao wa kawaida, wanafiki wao, na wale ambao sio wanafiki miongoni mwao. Basi, wanachuoni miongoni mwao, wao wanashikamana na upotovu walio nao. Nao watu wa kawaida, wanawaiga wao, na hawana ufahamu. Hivyo basi, nyinyi hamna matumaini yoyote katika makundi haya mawili.