Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sūrah 2

Al-Baqara

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 284

لِّلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ۗ وَإِن تُبْدُوا۟ مَا فِىٓ أَنفُسِكُمْ أَوْ تُخْفُوهُ يُحَاسِبْكُم بِهِ ٱللَّهُ ۖ فَيَغْفِرُ لِمَن يَشَآءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَآءُ ۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ 284

{284} Mola Mtukufu anajulisha ujumla wa ufalme wake juu ya wakazi wa mbinguni na ardhini. Na kuenea kwa elimu yake yale waliyoyaweka wazi waja wake na yale waliyoyaficha katika nafsi zao, na kwamba atawahesabu kwayo. "Kisha atamsamehe amtakaye." Naye ni yule anayerejea kwa Mola wake Mlezi na kutubia kwake. "Basi Yeye hakika, ni Mwenye kuwasamehe wanaotubia kwake." "Na amwadhibu amtakaye," naye ni yule anayeendelea kufanya maasia kwa ndani yake na nje yake. Na Aya hii haipingani na hadithi zilizokuja kuhusu kumsamehe alichojisemeza mja ndani ya nafsi yake, maadamu hakufanya wala kuzungumza. Hayo ni mawazo ambayo yanapita ndani ya nafsi, ambayo hasifiki mja kwayo wala hayaazimii. Ama hapa, ni maazimio aliyokwisha yaamulia na sifa zilizoimarika katika nafsi yake, na sifa nzuri na sifa mbaya. Na ndiyo maana akasema, "yaliyomo katika nafsi zenu" yani yaliyokwisha makinika ndani yake na yakaimarika miongoni mwa maazimio na sifa. kukaa ndani yake na kuimarika kutokana na maazimio na maelezo. Na akajulisha kuwa Yeye "ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu." Na katika ukamilifu wa uwezo wake, ni kuwahesabu viumbe na kufikisha wanachostahiki katika malipo na adhabu.