Al-Baqara
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
فَلَمَّا فَصَلَ طَالُوتُ بِٱلْجُنُودِ قَالَ إِنَّ ٱللَّهَ مُبْتَلِيكُم بِنَهَرٍ فَمَن شَرِبَ مِنْهُ فَلَيْسَ مِنِّى وَمَن لَّمْ يَطْعَمْهُ فَإِنَّهُۥ مِنِّىٓ إِلَّا مَنِ ٱغْتَرَفَ غُرْفَةًۢ بِيَدِهِۦ ۚ فَشَرِبُوا۟ مِنْهُ إِلَّا قَلِيلًا مِّنْهُمْ ۚ فَلَمَّا جَاوَزَهُۥ هُوَ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مَعَهُۥ قَالُوا۟ لَا طَاقَةَ لَنَا ٱلْيَوْمَ بِجَالُوتَ وَجُنُودِهِۦ ۚ قَالَ ٱلَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَـٰقُوا۟ ٱللَّهِ كَم مِّن فِئَةٍ قَلِيلَةٍ غَلَبَتْ فِئَةً كَثِيرَةًۢ بِإِذْنِ ٱللَّهِ ۗ وَٱللَّهُ مَعَ ٱلصَّـٰبِرِينَ 249 وَلَمَّا بَرَزُوا۟ لِجَالُوتَ وَجُنُودِهِۦ قَالُوا۟ رَبَّنَآ أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَٱنصُرْنَا عَلَى ٱلْقَوْمِ ٱلْكَـٰفِرِينَ 250
{249 - 250} "Hakika, Mwenyezi Mungu atawajaribu kwa mto." Mtakaopita karibu nao wakati mtakapokuwa mnahitaji maji, "atakayekunywa humo, si pamoja nami" yani asinifuate. Kwa sababu, hiyo ni dalili ya uchache wa subira yake na wingi wa kutosubiri kwake. "Na yule asiyeyaonja, basi huyo atakuwa pamoja nami" kwa sababu ya ukweli wake na subira yake. "Isipokuwa yule atakayeteka humo kiasi ya kitanga cha mkono wake" yani huyo ameruhusiwa hilo. Na walipoufikia mto huo, nao walikuwa wanahitaji maji, wote wakanywa kutoka humo. "Wachache tu miongoni mwao" hao walisubiri na hawakunywa. "Na alipovuka mto yeye na wale walioamini pamoja naye, wakasema" yani waoga au wale waliovuka ng'ambo. "Leo hatumwezi Jaluti (Goliati) na majeshi yake." Ikiwa wanaosema ni wale waoga, basi hii ni kauli ambayo kwayo wanaifanya kuwa ndiyo sababu ya woga wao. Na ikiwa wanaosema ni wale waliovuka ng'ambo pamoja na Talut, basi ni kama walipatwa na namna fulani ya udhaifu katika nafsi zao. Lakini wenye imani kamili wakawatia moyo wawe imara na waende kupambana, waliposema: "Ni makundi mangapi madogo yameshinda makundi makubwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri" kwa msaada wake, na kutia kwake nguvu, na nusura yake. Kwa hivyo wakawa imara na wakasubiri ili kupigana vita na adui yao Jalut (Goliathi) na majeshi yake.