Al-Baqara
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
وَإِذَا طَلَّقْتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا تَعْضُلُوهُنَّ أَن يَنكِحْنَ أَزْوَٰجَهُنَّ إِذَا تَرَٰضَوْا۟ بَيْنَهُم بِٱلْمَعْرُوفِ ۗ ذَٰلِكَ يُوعَظُ بِهِۦ مَن كَانَ مِنكُمْ يُؤْمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ ۗ ذَٰلِكُمْ أَزْكَىٰ لَكُمْ وَأَطْهَرُ ۗ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ 232
{232} Haya ni maneno kwa wasimamizi wa mwanamke aliyetalikiwa talaka chini ya tatu. Anapotoka katika eda na akataka kwamba mumewe amuoe, na (mwanamke) akaridhia hilo, basi hairuhusiwi kwa msimamizi wake kama vile baba na wengineo kumzuia kumuoa kwa sababu ya kuwa na hasira kubwa naye; na kuchukizwa na alichokifanya cha ile talaka ya kwanza. Na akataja kwamba anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, imani yake humzuia na hilo. Na hayo, "ni bora zaidi kwenu na safi kabisa" na nzuri zaidi kuliko vile anavyodhania msimamizi huyu. Kwamba kutomwozesha huyu mwanamume ndiyo rai iliyo sawa na inayofaa, na kwamba akabiliwe kwa ile talaka yake ya kwanza kwa kutomwozesha, kama ilivyo ada ya wenye starehe, wenye kutakabari. Na ikiwa anadhania kuwa masilahi yako katika kutomwozesha, basi Mwenyezi Mungu "anajua, na nyinyi hamjui". Kwa hivyo, fuateni amri ya yule anayeyajua masilahi yenu, anayeyataka, mwenye uwezo juu yake, na anayeyarahisisha kwa kwa njia ambazo mnazijua, na nyinginezo (msizojua). Katika Aya hii kuna dalili ya kuwa ni lazima kuwepo msimamizi katika nikaha. Kwa sababu aliwakataza wasimamizi kuzuia, na wala hawakatazi isipokuwa jambo ambalo lipo chini ya uendeshaji wao ambalo wana haki ndani yake. Kisha yeye Mtukufu akasema: