Al-Baqara
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
وَإِن كُنتُمْ فِى رَيْبٍ مِّمَّا نَزَّلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا فَأْتُوا۟ بِسُورَةٍ مِّن مِّثْلِهِۦ وَٱدْعُوا۟ شُهَدَآءَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ 23
(23) Na hii ni dalili ya kiakili juu ya ukweli wa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake na usahihi wa yale aliyoyaleta. Akasema: “Na ikiwa - enyi kundi la wale wanaompinga Mtume, wanaokataa ulinganizi wake, wanaodai kuwa ni mwongo - mna shaka, mchanganyiko juu ya hayo tuliyomteremshia mja wetu; je, ni kweli au ni linginelo? Basi hapa kuna jambo la uadilifu lenye upambanuzi baina yenu na yeye, nalo ni kuwa yeye ni binadamu kama nyinyi, sio wa jamii nyingine. Nanyi mnamjua tangu alipoinukia kati yenu, hawezi kuandika wala kusoma. Kisha akawajia na kitabu anachodai kuwa kimetoka kwa Mwenyezi Mungu. Nanyi mkasema: Hakika yeye amekitunga na akakizua. Kwa hivyo, ikiwa mambo ni kama mnavyosema, basi leteni sura moja ya mfano wake. Na tafuteni msaada kutoka kwa yeyote mnayeweza katika wasaidizi wenu na mashahidi wenu, kwani hili ni jambo jepesi kwenu. Hasa kwamba nyinyi ni watu wa ufasaha na usemi, na uadui mkubwa kwa Mtume. Hivyo, mkija na sura mfano wake, basi ni kama mlivyodai. Na msipoleta sura mfano wake, na mkashindwa kabisa [na wala hamtaleta sura mfano wake. Lakini tathmini hii ni katika mlango wa kufanya uadilifu tu na kuendelea kwenda ni nyinyi.] Basi hii ni ishara kubwa, na dalili ya wazi na ya peupe juu ya ukweli wake (Mtume), na ukweli wa aliyokuja nayo. Basi ni wajibu juu yenu kumfuata, na kuepukana na Moto ambao ulifika katika ukubwa na ukali wa joto lake kiwango kwamba kuni zake ni watu na mawe, siyo kama moto wa duniani ambao unawashwa tu kwa kuni. Na moto huu ulioelezwa umetengenezwa na kutayarishwa kwa ajili ya wanaomkufuru Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Hivyo, jihadharini na kumkufuru Mtume wake baada ya kukubainikieni kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.