Al-Baqara
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ٱشْتَرَوُا۟ ٱلضَّلَـٰلَةَ بِٱلْهُدَىٰ فَمَا رَبِحَت تِّجَـٰرَتُهُمْ وَمَا كَانُوا۟ مُهْتَدِينَ 16
Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema akifichua uhakika wa hali yao:
(16) "Hao", yaani wanafiki wanaosifika kwa sifa hizi "ndio walionunua upotovu kwa uwongofu." Yaani, walitaka sana upotovu kama vile mnunuzi anavyotaka sana bidhaa, ambayo - kwa sababu ya kuitaka (kuipenda) - anaitolea mali yenye thamani kubwa. Na huu ni katika mifano mizuri kabisa, kwani (mnafiki) aliufanya upotovu ambao ndiyo shari kubwa zaidi kuwa bidhaa. Na akaufanya uwongofu ambao ndio kutengenea kukubwa zaidi pahali pa bei, kwa hivyo wakautoa uwongofu kwa kuukataa katika kuutaka upotovu. Basi hii ndiyo biashara yao; nayo ndiyo biashara mbaya mno. Na haya ndiyo mapatano yao; nayo ndiyo mapatano mabaya mno. Na ikiwa mwenye kutoa dinari moja na kuchukua dirhamu moja ni mwenye hasara, basi atakuwaje mwenye kutoa johari na kuchukua dirhamu moja badala yake? Na vipi mwenye kutoa uwongofu badala ya upotofu, na akachagua uovu badala ya kufaulu (furaha), na akapenda mambo duni na akayaacha ya juu? Basi biashara yake haikupata faida, bali alipata hasara kubwa sana ndani yake. Hao ndio waliozihasiri nafsi zao na ahali zao Siku ya Kiyama. Tambueni kuwa hiyo ndiyo hasara iliyo dhahiri. Na kauli yake "wala hawakuwa wenye kuongoka" ni kusisitiza upotofu wao, na kwamba hawakupata chochote katika uwongofu. Na hizi ndizo sifa zao mbaya. Kisha akataja mfano wao [unaoziweka wazi (hizi sifa) uwazi wa juu zaidi], akasema: