Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sūrah 2

Al-Baqara

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 157

أُو۟لَـٰٓئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَٰتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ ۖ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُهْتَدُونَ 157

157) “Hao” waliosifika kwa subira iliyotajwa, “juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao Mlezi.” Yani sifa na utajo wa hali zao, “na rehema” kubwa. Na katika rehema yake juu yao ni kuwa aliwawezesha kuwa na subira ambayo kwayo wakapata malipo kamilifu, “na hao ndio walioongoka.” Ambao waliijua haki. Nayo mahali hapa ni kujua kwao kwamba wao ni wa Mwenyezi Mungu na kwamba kwake Yeye watarejea. Na wakaifanyia kazi. Nako huko wakaifanyia kazi kwao hapa ni ile subira yao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na Aya hii inaashiria kwamba asiyekuwa na subira, atakuwa na kinyume cha walichonacho. Basi atapata kashfa kutoka kwa Mwenyezi Mungu na adhabu, na upotofu na hasara. Basi ni kubwa vipi tofauti iliyopo kati ya haya makundi mawili! Na ni machovu machache yaliyoje ya wenye subira, na shida kubwa iliyoje ya wanaohuzunika. Aya hizi mbili zinajumuisha kutuliza nafsi kabla ya misimba kutokea ili iwe (misiba) rahisi na mepesi inapotekea. Na kubainisha yale inayokabiliwa (misiba) kwayo inapotokea, nayo ni subira. Na kubainisha yale yanayosaidia katika subira kile walichonacho wenye subira katika malipo. Na inajulikana hali ya asiyekuwa na subira kwa kinyume cha hali ya mwenye subira. Na kwamba majaribio na mitihani ni mwendo wa Mwenyezi Mungu ambao ulikwisha pita, na hutapata mabadiliko katika mwendo wa Mwenyezi Mungu. Na pia kuna kubainisha aina za misiba.