Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sūrah 2

Al-Baqara

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 137

فَإِنْ ءَامَنُوا۟ بِمِثْلِ مَآ ءَامَنتُم بِهِۦ فَقَدِ ٱهْتَدَوا۟ ۖ وَّإِن تَوَلَّوْا۟ فَإِنَّمَا هُمْ فِى شِقَاقٍ ۖ فَسَيَكْفِيكَهُمُ ٱللَّهُ ۚ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ 137

(137) Yani ikiwa Watu wa Kitabu wataamini kama mnavyoamini nyinyi, enyi kundi la Waumini, katika Mitume wote na Vitabu vyote. Ambao wa kwanza kuingia miongoni mwao na anayefaa zaidi kuwa wa mwisho wao, na mbora wao ni Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake - na Qur-ani, na wajisalimishe kwa Mwenyezi Mungu peke yake. Wala wasitofautishe yeyote kati ya Mitume "itakuwa kweli wameongoka" kwenye njia iliyonyooka inayofikisha kwenye Pepo zenye neema. Yani hawana njia yoyote ya kuongoka isipokuwa kwa imani hii. Sio kama walivyodai kwa kauli yao: Kuweni Mayahudi au Wakristo ndio mtaongoka. Basi wakadai kuwa uwongofu ni mahususi katika yale waliyoko juu yake. Na uongofu ni kujua haki na kuitendea matendo mema. Na kinyume chake ni kupotea mbali na elimu, na kupotea mbali na matendo (mema) baada ya kuyajua. Nako ndiko kupinga walikokuwa nako walipogeuka na kukengeuka. hivyo, mpinzani ni yule ambaye anakuwa upande mmoja, naye Mwenyezi Mungu na Mtume wake katika upande mwingine. Na inalazimu kutokana na upinzani, kuwepo uadui mkubwa ambao unalazimu kufanya iwezekanavyo kumuudhi Mtume. Kwa sababu ya hilo, Mwenyezi Mungu alimwahidi Mtume wake kwamba atamtosheleza kutokana nao, kwa maana, Yeye ndiye "Msikizi" wa sauti zote katika lugha mbalimbali kwa mahitaji tofauti tofauti. "Mwenye elimu (Mjuzi)" wa yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao katika yaliyofichika na yale yanayoonekana, ya dhahiri na ya ndani (yaliyofichika). Na ikiwa hivyo, basi Mwenyezi Mungu atakulinda na shari yao. Na Mwenyezi Mungu alimtimizia Mtume wake ahadi yake, na akampa nguvu juu yao mpaka akawauwa baadhi yao, na akawateka baadhi yao, na akawatoa baadhi yao, na akawakimbiza kila pande zote. Basi ndani yake kuna muujiza miongoni mwa miujiza ya Qur-ani, ambao ni kupeana habari ya jambo kabla halijatokea, kisha likatokea kwa mujibu wa ilivyosema.