Al-Baqara
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَقُولُوا۟ رَٰعِنَا وَقُولُوا۟ ٱنظُرْنَا وَٱسْمَعُوا۟ ۗ وَلِلْكَـٰفِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ 104
(104) Waislamu walikuwa wakisema wanapomwongelesha Mtume wakati wanaposoma jambo la dini "Raa'inaa", yani tuchunge hali zetu. Nao walikuwa wakikusudia kwa hayo maana yake sahihi. Nao Mayahudi walikuwa wakitaka kwayo maana potovu. Kwa hivyo, wakaichukua fursa hiyo na wakaanza kumsemesha Mtume kwa hayo na wakakusudia maana potofu. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawakataza Waumini kutokana na hili neno, ili kuufunga mlango huu. Ndani yake kuna katazo la linaloruhusika ikiwa ni njia ya kufikisha kwa la haramu. Na ndani yake kuna adabu na matumizi ya maneno ambayo hayamaanishi isipokuwa uzuri, na kutokuwa na maneno machafu. Pia kuacha maneno mabaya au yenye aina fulani ya mkanganyiko na yenye uwezekano wa kumaanisha jambo lisilofaa. Kwa hivyo, akawaamrisha neno lisiloweza kumaanisha isipokuwa uzuri, akasema "na semeni: "Ndhurna (Tuangalieni)” kwa maana linatosha kufikia yaliyokusudiwa bila ya linalotahadharishwa. ”Na sikieni!" Na hapa hakutaja kinachosikilizwa, ili lijumuishe aliyoamrishwa asikilize, ndio iingie ndani yake kusikiliza Qur-ani na kusikiliza Sunnah, ambayo ndiyo hekima kimatamshi na kimaana, na kuitikia. Kwa hivyo, ndani yake kuna adabu na utiifu. Kisha akawatishia makafiri adhabu chungu iumizayo.