Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · Ar-Ra'd
Sūrah 13

Ar-Ra'd

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 1

الٓمٓر ۚ تِلْكَ ءَايَـٰتُ ٱلْكِتَـٰبِ ۗ وَٱلَّذِىٓ أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ٱلْحَقُّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يُؤْمِنُونَ 1

{1} Yeye Mtukufu anajulisha kuwa Qur’ani hii ni ishara za Kitabu zinazoonyesha kila wanachokihitaji waja katika misingi na matawi ya Dini, na kwamba yale yaliyoteremshwa kwa Mtume kutoka kwa Mola wake Mlezi ndiyo haki iliyo wazi. Kwa sababu habari zake ni za ukweli na amri zake na makatazo yake ni ya uadilifu, yanayoungwa mkono na ushahidi na hoja za mkato. Kwa hivyo mwenye kukielekea kwa kukisoma, basi anakuwa miongoni mwa wenye elimu juu ya haki ambao elimu yao hiyo inawasababishia kufanya kile ambacho Mwenyezi Mungu anapenda. “Lakini wengi wa watu [hawaamini]” katika Qur’ani hii: ima kwa sababu ya ujinga na kupeana tu mgongo na kutoijali, au kwa sababu ya ukaidi na dhuluma. Na ndiyo sababu hiyo, wengi wa watu hawafaidiki nayo, kwa sababu hawana sababu ya kuwafanya wafaidike.