الشرح
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَإِذَا فَرَغْتَ فَٱنصَبْ ٧ وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَٱرْغَب ٨
{7 - 8} Kisha [Mwenyezi Mungu] akamwamrisha Mtume wake kwanza, na Waumini kwa kumfuata, kumshukuru na kutimiza wajibu wa neema zake, akasema: "Na ukipata faragha, fanya juhudi" yaani unapomaliza shughuli zako, na kukawa hakuna kitu kinachobaki moyoni mwako cha kuuzuia, basi jitahidini katika ibada na dua, "Na Mola wako Mlezi" peke yake "ndio mshughulikie." Yaani, kuwa na shauku kubwa ya kutaka kuitikiwa dua zako, na usiwe miongoni mwa wale ambao wanapomaliza, wanafanya mchezo na wakampa mgongo Mola wao Mlezi na pia utajo wake, basi ukawa miongoni mwa waliohasirika. Na imesemwa kwamba maana yake ni kwamba unapomaliza swala na ukaikamilisha, basi jitahidi katika kuomba dua, na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie kwa kuomba unayoyataka. Aliyeisema kauli hii iliitumia kama ushahidi wa uhalali wa kuomba dua na kumtaja Mwenyezi Mungu baada ya swala za lazima. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye hilo zaidi.
Imekamilika, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.