التوبة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يَعْتَذِرُونَ إِلَيْكُمْ إِذَا رَجَعْتُمْ إِلَيْهِمْ ۚ قُل لَّا تَعْتَذِرُوا۟ لَن نُّؤْمِنَ لَكُمْ قَدْ نَبَّأَنَا ٱللَّهُ مِنْ أَخْبَارِكُمْ ۚ وَسَيَرَى ٱللَّهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُۥ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَـٰلِمِ ٱلْغَيْبِ وَٱلشَّهَـٰدَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ٩٤
{94} Alipotaja kusalia nyuma kwa wanafiki matajiri, na kwamba hawana udhuru wowote, akajulisha kwamba watawatoa udhuru "mtakapowarudia" kutoka katika vita vyenu. "Sema" uwaambie: "Msitoe udhuru, hatutawaamini;" yaani, hatutawasadiki katika kutoa udhuru kwenu kwa uongo. “Mwenyezi Mungu amekwisha tujulisha habari zenu,” naye ndiye mkweli zaidi katika anayoyasema; basi haikubakia faida yoyote katika kuomba udhuru. Kwa sababu wanatoa udhuru kinyume na kile ambacho Mwenyezi Mungu alijulisha juu yao, na haiwezekani kwamba wao ni wakweli katika kile kinachopingana na habari za Mwenyezi Mungu, ambayo ndiyo kiwango cha juu zaidi cha ukweli. "Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wataviona vitendo vyenu" katika dunia hii. Kwa sababu matendo ndiyo mizani ya kutofautisha kati ya ukweli na uongo. Na ama maneno matupu, hayo hayana ushahidi wowote ndani yake juu ya hayo. "Kisha mtarudishwa kwa Mjuzi wa ya siri na ya dhahiri” ambaye hakimfichiki chochote chenye kufichika, "naye atawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda" miongoni mwa heri na maovu, na atawalipa kwa uadilifu wake au kwa fadhila yake bila ya kuwadhulumu uzito wa chembe.