التوبة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَجَآءَ ٱلْمُعَذِّرُونَ مِنَ ٱلْأَعْرَابِ لِيُؤْذَنَ لَهُمْ وَقَعَدَ ٱلَّذِينَ كَذَبُوا۟ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ ۚ سَيُصِيبُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ٩٠
{90} Yeye Mtukufu anasema, “Na walikuja wenye kutoa udhuru miongoni mwa Mabedui ili wapewe ruhusa.” Yaani, wale waliozembea na kutofanya namna ipasavyo miongoni mwao kuhusiana na kutoka kwenda vitani wakaja ili wapewe ruhusa ya kuacha jihadi, bila ya kujali kuomba udhuru kwa sababu ya ugumu wao na ukosefu wa staha wao, na kuja kwao kwa sababu ya imani yao dhaifu waliyo nayo. Na ama wale waliomkadhibisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake miongoni mwao, wao walikaa na wakaacha kuomba udhuru kabisa. Na inawezekana kwamba maana ya kauli yake: "wenye kutoa udhuru;" yaani, wale walio na udhuru walimjia Mtume - rehema na amani zimshukie - ili awape ruhusa, na ni katika kawaida yake kumpa ruhusa mwenye udhuru. “Na wakakaa wale waliomdanganya Mwenyezi Mungu na Mtume wake,” katika madai yao kwamba wameamini imani inayolazimu kutoka kwenda vitani, lakini hawakufanya hivyo. Kisha akawaahidi adhabu kwa kauli yake “itawafika wale waliokufuru miongoni mwao adhabu chungu.” Katika dunia na Akhera.