انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · التوبة
السورة ٩

التوبة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٨

كَيْفَ وَإِن يَظْهَرُوا۟ عَلَيْكُمْ لَا يَرْقُبُوا۟ فِيكُمْ إِلًّا وَلَا ذِمَّةً ۚ يُرْضُونَكُم بِأَفْوَٰهِهِمْ وَتَأْبَىٰ قُلُوبُهُمْ وَأَكْثَرُهُمْ فَـٰسِقُونَ ٨

Na ndiyo maana akasema

{8} Yaani, "Vipi" washirikina watakuwa na ahadi na agano kwa Mwenyezi Mungu, "Na" hali ni kwamba "wakiwa na ushindi dhidi yenu" kwa nguvu na wakawa na mamlaka hawawahurumii na "hawachungi kwenu udugu wala ahadi." Yaani, si dhima wala jamaa wa nasaba, wala hawamchi Mwenyezi Mungu kuhusiana nanyi. Bali wanawatia adhabu mbaya zaidi. Basi hii ndiyo hali yenu kwao ikiwa watakuwa washindi, wala yasiwadanganye yale wanayoamiliana nanyi kwayo wakati wanapokuwa wanawahofu. Wao kwa hakika, "Wanawafurahisha kwa midomo yao tu, lakini nyoyo zao zinakataa hayo" ya kuwaelekea nyinyi na kuwapenda. Bali wao ni maadui wa kweli, wanaowachukia kwa ukweli. "Na wengi wao ni wavukao mipaka;" hawana dini wala maadili.