التوبة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لَقَدِ ٱبْتَغَوُا۟ ٱلْفِتْنَةَ مِن قَبْلُ وَقَلَّبُوا۟ لَكَ ٱلْأُمُورَ حَتَّىٰ جَآءَ ٱلْحَقُّ وَظَهَرَ أَمْرُ ٱللَّهِ وَهُمْ كَـٰرِهُونَ ٤٨
{48} Kisha akataja kuwa tayari walikwisha fanya maovu hapo awali, kwa hivyo akasema "Hakika, walikwisha taka fitina tangu zamani." Yaani, wakati mlipohamia Madina, walifanya juhudi zao zote “na wakakugeuzia mambo." Yaani, walizigeuza fikira, na wakatumia hila katika kubatilisha wito wako, na kuiangusha dini yenu, na hawakupuuza chochote katika kufanya hivyo "mpaka ikaja haki na ikadhihirika amri ya Mwenyezi Mungu hali ya kuwa wao wamechukia." Kwa hivyo, njama zao zikabatilika, na batili yao ikapotelea mbali. Basi mfano wa hawa wanastahiki zaidi kwamba Mwenyezi Mungu anawatahadharisha waja wake Waimuni dhidi yao, na kwamba Waumini wasijali na kusalia kwa hao nyuma yao.