التوبة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يَوْمَ يُحْمَىٰ عَلَيْهَا فِى نَارِ جَهَنَّمَ فَتُكْوَىٰ بِهَا جِبَاهُهُمْ وَجُنُوبُهُمْ وَظُهُورُهُمْ ۖ هَـٰذَا مَا كَنَزْتُمْ لِأَنفُسِكُمْ فَذُوقُوا۟ مَا كُنتُمْ تَكْنِزُونَ ٣٥
{35} Kisha akaitafsiri kwa kauli yake "Siku zitakapotiwa moto" yaani, zitakapotiwa mali zao moto {katika moto wa Jahannam}: na kila dinari au dirhamu ikatiwa moto kando kando, "na kwazo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao" katika Siku ya Qiyama. Kila zikiwa baridi, zinarudishwa, katika siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu hamsini. Na wataambiwa wakikaripiwa na kulaumiwa, "Haya ndiyo mliyozilimbikia nafsi zenu. Basi onjeni mliyokuwa mkilimbika." Nasi hatukuwadhulumu, lakini mlijidhulumu wenyewe, na mkaziadhibu kwa milimbiko hii. Na Mwenyezi Mungu alitaja katika aya mbili hizi kupotoka kwa mwanadamu katika mali yake. Na hilo ni kwa moja ya mambo mawili: Ima kwa kuitumia katika batili ambayo haimletei faida yoyote, bali hayampati kutoka kwayo isipokuwa madhara tupu. Na hili kama vile kutia mali katika maasia na matamanio ambayo hayasaidii katika kumtii Mwenyezi Mungu, na kuitia ili kuzuia njia ya Mwenyezi Mungu. Na ima aizuie mali yake asiitoe katika mambo ya wajibu. Na kukataza kitu fulani ni kuamriwa kinyume chake.