انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · التوبة
السورة ٩

التوبة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٧

ثُمَّ يَتُوبُ ٱللَّهُ مِنۢ بَعْدِ ذَٰلِكَ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ ۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ٢٧

{27} "Kisha baada ya hayo Mwenyezi Mungu atamkubalia toba amtakaye." Na Mwenyezi Mungu akakubali toba ya wengi wa wale vita vilikuwa dhidi yao, na wakamjia Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie hali ya kuwa ni Waislamu, huku wametubia. Kwa hivyo, akawarudishia wanawake wao na wana wao "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusitiri dhambi, Mwenye kurehemu." Yaani ni mwenye kusitiri dhambi kwa ukunjufu, na rehema za jumla, anasamehe dhambi kubwa kwa wanaotubia, na anawarehemu kwa kuwawezesha kutubia na kuwa watiifu, na kuachilia mbali makosa yao, na kukubali toba zao, basi kamwe asikate tamaa yeyote yule juu ya rehema zake na kusitiri dhambi kwake, hata kama atafanya katika dhambi na uhalifu kile alichofanya.