التوبة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
مَا كَانَ لِلْمُشْرِكِينَ أَن يَعْمُرُوا۟ مَسَـٰجِدَ ٱللَّهِ شَـٰهِدِينَ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِم بِٱلْكُفْرِ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَـٰلُهُمْ وَفِى ٱلنَّارِ هُمْ خَـٰلِدُونَ ١٧
{17} Yeye Mtukufu anasema: "Haikuwa;" yaani, haifai wala haiendani "kwa washirikina kwamba waiimarishe misikiti ya Mwenyezi Mungu" kwa ibada, na sala na aina nyinginezo za utii, ilhali wao wanashuhudia na wanakiri ukafiri juu ya nafsi zao kwa ushahidi wa hali zao na maumbile yao, na kujua kwa wengi miongoni mwao kwamba wako katika ukafiri na batili. Basi ikiwa "wanazishuhudia nafsi zao wenyewe ukafiri" na kutokuwa na imani ambayo ndiyo sharti la kukubaliwa matendo, basi vipi wanadai kwamba wanaiimarisha misikiti ya Mwenyezi Mungu, na msingi wao hauko, na matendo yao ni batili? Na ndiyo maana akasema: "Hao matendo yao yaliharibika;" yaani, yalibatilika na yakapotea. "Na katika Moto wao watadumu."