انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · التوبة
السورة ٩

التوبة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٢

وَإِن نَّكَثُوٓا۟ أَيْمَـٰنَهُم مِّنۢ بَعْدِ عَهْدِهِمْ وَطَعَنُوا۟ فِى دِينِكُمْ فَقَـٰتِلُوٓا۟ أَئِمَّةَ ٱلْكُفْرِ ۙ إِنَّهُمْ لَآ أَيْمَـٰنَ لَهُمْ لَعَلَّهُمْ يَنتَهُونَ ١٢

{12} Yeye Mtukufu anasema baada ya kutaja kwamba wale waliofunga agano miongoni mwa washirikina ikiwa watanyooka katika agano lao, basi nyinyi wanyookeeni pia kwa kuwatimizia. "Na wakivunja viapo vyao baada ya agano lao;" yaani, wakivivunja na kuvifungua, na wakapigana nanyi au wakawasaidia wengine kuwapiga nyinyi au wakawapunguzia kitu, "na wakaitia dosari Dini yenu;" yaani, wakaishutumu na kuifanyia masihara. Na inaingia katika hilo aina zote za kutia dosari zinazoelekezwa kwa dini au Qur-ani, "basi piganeni na viongozi wa ukafiri" yaani, viongozi wake, na marais wanaoitia dosari Dini ya Mwingi wa Rehema, wanaoinusuru dini ya Shetani. Na aliwataja hawa hasa kwa sababu ya ukubwa wa uhalifu wao na kwa sababu wengineo wanawafuata hawa tu, na ili kuonyesha kwamba yeyote anayeitia dosari Dini, na akasimama mbele ili kuikataa, basi yeye ni miongoni mwa viongozi wa ukafiri. "Hakika hao hawana viapo vya kweli" yaani, hawana ahadi ya kweli wala maagano wanayoshikamana na jambo la kuyatimiza. Bali hawajaacha kufanya uhaini, na kuvunja agano, na hawaaminiki. "Huenda" katika kupigana kwenu nao "wakaacha" kuitia dosari dini yenu, na huenda wakaingia ndani yake.