التوبة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لَّقَد تَّابَ ٱللَّهُ عَلَى ٱلنَّبِىِّ وَٱلْمُهَـٰجِرِينَ وَٱلْأَنصَارِ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُ فِى سَاعَةِ ٱلْعُسْرَةِ مِنۢ بَعْدِ مَا كَادَ يَزِيغُ قُلُوبُ فَرِيقٍ مِّنْهُمْ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّهُۥ بِهِمْ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ ١١٧
{117} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba katika upole wake na wema wake "alikwisha kubali toba ya Nabii” Muhammad -rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - "na Wahajiri na Ansari.” Akawasamehe makosa yao na akawapa mazuri mengi, na akawapandisha hadi daraja za juu zaidi. Na hayo ni kwa sababu ya kutenda kwao matendo magumu, na ndiyo maana akasema: "waliomfuata katika saa ya ugumu.” Yaani, walitoka pamoja naye kwenda kupigana vita na maadui wao katika vita vya Tabuk. Na hilo lilikuwa katika joto kali, na upungufu wa masurufu na vipando, na idadi nyingi ya maadui wao, jambo linalopelekea mtu kusalia nyuma. Basi wakaomba msaada wa mwenyezi Mungu, na wakafanya hivyo "baada ya kwamba nyoyo za kundi miongoni mwa zilikuwa zimekaribia kukengeuka.” Yaani, nyoyo zao kugeuka na kuelekea kwenye upole juu ya maadui na utulivu, lakini Mwenyezi Mungu akawaimarisha na amewaunga mkono na akawatia nguvu. Na kukengeuka kwa moyo ni kutoka kwake katika njia iliyonyooka. Na ikiwa kupotoka huko ni katika msingi wa dini, basi hilo linakuwa ni kufuru. Na kama ni katika sheria zake, basi kunakuwa kulingana na sheria hiyo ambayo amepotoka kutoka kwayo: Ima hakuifanya ipasavyo, au aliifanya kwa njia ambayo si ya kisheria. Na kauli yake, “Basi akakubali toba yao. Hakika Yeye kwao ni Mpole, Mwenye kurehemu.” Na katika upole wake na rehema yake ni kwamba aliwaneemesha kufanya toba, na akaikubalia kutoka kwao, na akawaimarisha juu yake.