التوبة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَفَمَنْ أَسَّسَ بُنْيَـٰنَهُۥ عَلَىٰ تَقْوَىٰ مِنَ ٱللَّهِ وَرِضْوَٰنٍ خَيْرٌ أَم مَّنْ أَسَّسَ بُنْيَـٰنَهُۥ عَلَىٰ شَفَا جُرُفٍ هَارٍ فَٱنْهَارَ بِهِۦ فِى نَارِ جَهَنَّمَ ۗ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ ١٠٩
{109} Kisha akapambanua baina ya misikiti kulingana na nia za watu wenyewe na kukubaliana kwake na ridha yake, akasema: "Je, mwenye kuweka msingi wa jengo lake juu ya uchaji utokao kwa Mwenyezi Mungu.” Yaani, kwa nia njema na ikhlasi, "radhi zake” kwamba aliafikiana na amri yake, kwa hivyo akajumuisha ikhlasi na kumfuata Mtume katika matendo yake. "Ni bora zaidi au mwenye kuweka msingi wa jengo lake juu ya ukingo wa shimo unaoporomoka.” Yaani, ambalo limekusanyika tayari kuporomoka. “Kwa hivyo ukaporomoka naye ndani ya Moto wa Jahannamu? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu madhalimu” kwa yale yenye masilahi ya dini yao na dunia yao.