التوبة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَقُلِ ٱعْمَلُوا۟ فَسَيَرَى ٱللَّهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُۥ وَٱلْمُؤْمِنُونَ ۖ وَسَتُرَدُّونَ إِلَىٰ عَـٰلِمِ ٱلْغَيْبِ وَٱلشَّهَـٰدَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ١٠٥
{105} Yeye Mtukufu Anasema: "Na waambie” wanafiki hawa: "Fanyeni" matendo yoyote mnayoyaona, na endeleeni katika batili yenu, na msidhani kuwa hayo yatafichika. "Na Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Waumini watayaona matendo yenu.” Yaani, hakuna budi kwamba matendo yenu yatabainika na yatakuwa wazi. "Na mtarudishwa kwa Mwenye kujua siri na dhahiri; basi naye atawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda;" ya heri na maovu. Na katika tishio hili na ahadi hii ya adhabu kali kwa mwenye kuendelea juu ya batili yake, na kuvuka kwake mipaka, na upotovu wake, na uasi wake. Na inawezekana kwamba maana yake ni hata mkifanya kiasi gani cha heri au uovu, Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwaona, na atamwonyesha Mtume wake na waja wake Waumini matendo yenu, hata kama yamefichika.