انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · البروج
السورة ٨٥

البروج

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٥

ذُو ٱلْعَرْشِ ٱلْمَجِيدُ ١٥

{15} "Mwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu." Yaani, mwenye Kiti cha Enzi kikubwa, ambacho katika ukubwa wake ni kwamba kimeenea mbingu, ardhi na mahali pa inapokanyaga miguu yake (Kursii). Kwani mahali hapo kwa kulinganisha na Kiti cha Enzi ni kama pete iliyotupwa katika jangwa kwa kulinganisha na ardhi iliyobaki. Na hapa Mwenyezi Mungu amekitaja Kiti cha Enzi kwa njia maalumu kwa sababu ya utukufu wake, na kwa sababu ndicho kiumbe maalumu zaidi kilicho karibu zaidi naye. Maana hii inatokea neno "Al-Majiid" likisomwa na kasra (herufi i) ili liwe sifa ya Kiti cha Enzi. Ama likisomwa na dhwamma (herufi u) basi linakuwa ni sifa ya Mwenyezi Mungu kwamba ni Mtukufu.