النازعات
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يَسْـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلسَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَىٰهَا ٤٢ فِيمَ أَنتَ مِن ذِكْرَىٰهَآ ٤٣ إِلَىٰ رَبِّكَ مُنتَهَىٰهَآ ٤٤
{42 - 44} Maana yake ni kwamba wanakuuliza wenye ukaidi wanaokadhibisha ufufuo "Saa (ya Kiyama)" na kwamba "itakuwa lini?" Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawajibu kwa kauli yake: "Una nini wewe hata uitaje?" Yaani, kuna faida gani kwako na kwao katika kuitaja na kujua muda wa kuja kwake? Hakuna natija katika hilo, na ndiyo sababu hii, kwa kuwa kujua kwa waja kuhusu Saa ya Kiyama hakuna masilahi yao ya kidini wala ya kidunia, bali masilahi yao ni katika kuwaficha wasiijue, basi akaficha elimu ya hilo mbali na viumbe vyote na akajiwekea Yeye tu elimu ya hilo, akasema: "Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake." Yaani, kwake ndiyo ujua wake unaishia, kama alivyosema katika Aya nyingine: “Wanakuuliza hiyo Saa (ya mwisho) itakuwa lini? Sema: Kuijua kwake kuko kwa Mola Mlezi wangu. Haidhihirishi hiyo kwa wakati wake ila Yeye."