انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النبإ
السورة ٧٨

النبإ

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٣١–٣٦

إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا ٣١ حَدَآئِقَ وَأَعْنَـٰبًا ٣٢ وَكَوَاعِبَ أَتْرَابًا ٣٣ وَكَأْسًا دِهَاقًا ٣٤ لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا كِذَّٰبًا ٣٥ جَزَآءً مِّن رَّبِّكَ عَطَآءً حِسَابًا ٣٦

{31 - 36} Mwenyezi Mungu alipotaja hali ya wahalifu, akataja mwisho wa wachamungu, akasema: "Hakika wacha Mungu." Yaani, wale waliojiepusha mbali na ghadhabu ya Mola wao Mlezi kwa kushikamana na kumtii na kujiepusha na kumuasi "wanastahiki kufuzu" kwa kupewa njia ya kutokea na kuokoka kutokana na kuwa mbali na Moto. Na katika kufuzu huko watakuwa na "Mabustani" yanayokusanya aina za miti inayong'aa kwa matunda, yapitayo mito kati yake, na hapa alizitaja zabibu hasa kwa sababu ya heshima yake na wingi wake katika bustani hizo. Na wana wake humo kulingana na zitakavyo nafsi zao nao ni "wake wazuri" barubaru ambao matiti yao hayajaanguka kutokana na ujana wao, nguvu zao na urembo wao, "waliolingana nao." Na wake wa rika moja na waume zao kwa kawaida huwa nahisi vizuri kuwa pamoja na waume zao na huwa wanaishi nao kwa uzuri. Na miaka hii ya rika moja ambayo ndio umri wao ni miaka thelathini na tatu ambayo ndiyo mzuri zaidi ya ujana. "Na bilauri zilizojaa" vinywaji vizuri, vyenye ladha nzuri zaidi kwa wanywao. "Hawatasikia humo upuuzi." Yaani, mazungumzo yasiyo na faida "wala uwongo" kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi. Isipokuwa maneno ya Salama, Salama." Na Mwenyezi Mungu aliwapa malipo haya makubwa kutokana na fadhila zake na ukarimu wake, "kipawa cha kutosha" kwa sababu ya matendo yao ambayo Mwenyezi Mungu aliwawezesha kuyafanya, na akawafanya hayo kuwa njia ya kufikia utukufu wake.