المرسلات
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَإِذَا ٱلنُّجُومُ طُمِسَتْ ٨ وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ فُرِجَتْ ٩ وَإِذَا ٱلْجِبَالُ نُسِفَتْ ١٠ وَإِذَا ٱلرُّسُلُ أُقِّتَتْ ١١ لِأَىِّ يَوْمٍ أُجِّلَتْ ١٢ لِيَوْمِ ٱلْفَصْلِ ١٣ وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا يَوْمُ ٱلْفَصْلِ ١٤
{8 - 14} Ikitokea, kutakuwa na mabadiliko katika dunia na mambo ya kutisha sana ambayo yatasumbua nyoyo na kufanya uchungu kuwa mkubwa kiasi kwamba nyota zitazimika, zianguke kutoka mahali pake, nayo milima itapasuka iwe kama mavumbi yaliyotawanywa, na hiyo hiyo milima pamoja na ardhi viwe tambarare uwanda, hutaona humo mdidimio wala muinuko. Na siku hiyo ndiyo siku ambayo Mitume "watakapowekewa wakati wao” na iliahirishwa kwa ajili ya kufanya hukumu baina yao na mataifa yao, na ndiyo maana akasema: “Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo?" Huku ni kuuliza kwa njia ya kuonyesha ukuu, ukubwa na uzito wa jambo hili. Kisha akajibu kwa kauli yake: "Kwa siku ya kupambanua!" Yaani, baina ya viumbe wao kwa wao, na kumfanyia kila mmoja wao mahesabu yake juu ya matendo yake.