انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المدثر
السورة ٧٤

المدثر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ١–٢

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلْمُدَّثِّرُ ١ قُمْ فَأَنذِرْ ٢

{1 - 2} Hapo awali ilitajwa kuwa al-Muzzammil na al-Muddaththir ni maneno yenye maana sawa, na kwamba Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume wake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - afanye bidii katika ibada zinazomfaa yeye tu na zile za kuwafaa wengine pia. Basi ikatangulia hapo awali kwamba ameamrishwa kufanya ibada bora zaidi zenye kumfaa yeye tu na kuwa na subira na juu ya maudhi ya watu wake, na hapa akamuamuru kutangaza wito wake na kutoa onyo waziwazi. Kwa hivyo akasema: "Simama" kwa bidii na kwa ukakamavu "uonye" watu kwa kauli na vitendo vinavyofanikisha yaliyokusudiwa na pia kubainisha hali ya kile kinachoonywa juu yake, ili hilo liitie zaidi kuachana nalo.