انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الجن
السورة ٧٢

الجن

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١

قُلْ أُوحِىَ إِلَىَّ أَنَّهُ ٱسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ ٱلْجِنِّ فَقَالُوٓا۟ إِنَّا سَمِعْنَا قُرْءَانًا عَجَبًا ١

{1} Yaani, "Sema" ewe Mtume uwaambie watu, "Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikiliza." Mwenyezi Mungu aliwaelekeza kwa Mtume wake ili wazisikie Aya zake; ili hoja ithibitike juu yao, na ili neema itimie juu yao, na ili wawe waonyaji kwa watu wao. Mwenyezi Mungu alimuamrisha Mtume wake kwamba asimulie habari yao hii kwawa watu, kwa sababu, walipoihudhuria, wakasema: 'Sikilizeni na mnyamaze.' Basi waliponyamaza, walielewa maana zake na uhakika wake ukafikia mioyoni mwao. 'Wakasema: Hakika sisi tumeisikia Qur-ani ya ajabu!" Yaani, ni moja ya maajabu ya thamani kubwa sana na mambo ya juu zaidi yatafutwayo.