انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الحاقة
السورة ٦٩

الحاقة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٥١

وَإِنَّهُۥ لَحَقُّ ٱلْيَقِينِ ٥١

{51} "Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini" juu ya viwango vya elimu. Kwani viwango vya juu kabisa vya elimu ni yakini, ambayo ni elimu thabiti isioyumba wala kuondoka. Nayo yakini ina viwango vitatu, kila kimoja ni cha juu zaidi kuliko cha kabla yake: cha kwanza ni elimu ya yakini, ambayo ni elimu inayopatikana kutokana na habari. Kisha jicho la yakini, ambayo ni elimu inayopatikana kwa kuona kwa macho. Kisha haki ya yakini, ambayo ni elimu inayopatikana kwa hisia ya ladha na kugusana nayo. Na hii Qur-ani ni yenye maelezo haya. Kwa maana elimu iliyomo ndani yake inayoungwa mkono na uthibitisho wa kukata na mambo ya uhakika na elimu ya kiimani iliyo ndani yake anayopata mwenye kuionja ni haki ya yakini.