انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الحاقة
السورة ٦٩

الحاقة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٤

كَذَّبَتْ ثَمُودُ وَعَادٌۢ بِٱلْقَارِعَةِ ٤

{4} Kisha akataja mfano wa hali zao zilizomo duniani na zinazoonekana humo, na hayo ni yale aliyowafikishia ya adhabu kali kwa mataifa walioasi, na akasema: "Thamudi na A'di waliukadhibisha." Hao ni makabila yanayojulikana, watu waliokuwa wakiishi Al-Hijr, ambao Mwenyezi Mungu aliwatumia Mtume wake, Saleh, amani iwe juu yake, ili awakataze shirki waliyokuwamo na awaamrishe kumpwekesha, lakini waliukataa mwito wake, wakamkadhibisha, na wakakanusha aliyoyasema kuhusu Siku ya Kiyama, ambayo ni tukio kuu litakaliowatisha sana viumbe kwa vitisho vyake. Basi wakakadhibisha A'di wa kwanza, watu waliokuwa wakiishi Hadhramaut, Mwenyezi Mungu alipomtuma kwao Mtume wake Hud, rehema na amani ziwe juu yake, akiwalingania kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, nao wakamkadhibisha na kuyakanusha yale aliyoyaeleza kuhusu kufufuliwa, kwa hivyo Mwenyezi Mungu akayaangamiza makundi hayo yote mawili kwa maangamizo ya haraka.