انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الحاقة
السورة ٦٩

الحاقة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ١١–١٢

إِنَّا لَمَّا طَغَا ٱلْمَآءُ حَمَلْنَـٰكُمْ فِى ٱلْجَارِيَةِ ١١ لِنَجْعَلَهَا لَكُمْ تَذْكِرَةً وَتَعِيَهَآ أُذُنٌ وَٰعِيَةٌ ١٢

{11 - 12} Miongoni mwao ni kaumu ya Nuhu; Mwenyezi Mungu aliwazamisha baharini maji yalipoufunika uso wa ardhi na kupanda juu ya sehemu zake zilizoinuka juu, na Mwenyezi Mungu akawaneemesha viumbe waliokuwepo baada yao kwamba - aliwachukua "katika kinachokwenda,", ambacho ni safina, walipokuwa katika viuno vya baba zao na mama zao, ambao Mwenyezi Mungu aliwaokoa. Basi mhimidini Mwenyezi Mungu, na mumshukuru yule aliyekuokoeni alipowaangamiza madhalimu, na zizingatieni Aya zake na ishara zake zinazonyesha upweke wake, na ndiyo maana akasema: "Ili tuyafanye hayo" Yaani, safina hiyo na mfano huo kuwa ni "waadhi kwenu " atakaokukumbusheni safina ya mwanzo iliyojengwa na kisa chake, na jinsi Mwenyezi Mungu alivyowaokolea humo wale waliomuamini na wakamfuata Mtume wake, na akawaangamiza watu wote waliokuwa kwenye ardhi. Kwa maana kitu sawia kinakumbusha asili yake. Na kauli yake: "Na kila sikio linalosikia liyahifadhi." Yaani: wenye akili wayafahamu, na wayajue makusudio yake na vipi ya kuyatumia kuwa ni ishara. Haya ni tofauti na watu wanaopeana mgongo, walioghafilika, watu wagumu wasio na akili ya utambuzi. Kwani wao hawafaidiki na Ishara za Mwenyezi Mungu. Kwa sababu wao hawaelewi kitu kutoka kwa Mwenyezi Mungu na hawazifikirii ishara zake.