انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الملك
السورة ٦٧

الملك

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٣

ٱلَّذِى خَلَقَ سَبْعَ سَمَـٰوَٰتٍ طِبَاقًا ۖ مَّا تَرَىٰ فِى خَلْقِ ٱلرَّحْمَـٰنِ مِن تَفَـٰوُتٍ ۖ فَٱرْجِعِ ٱلْبَصَرَ هَلْ تَرَىٰ مِن فُطُورٍ ٣

{3} "Aliyeumba mbingu saba kwa matabaka." Yaani, kila moja ikiwa juu ya nyenzake, na wala si tabaka moja tu, na akaziumba kwa uzuri mkubwa mno na ustadi wa hali ya juu. "Huoni tafauti yoyote katika uumbaji wa Mwingi wa Rehema." Yaani, huwezi kuona kasoro na upungufu. Na ikiwa upungufu haupo kwa namna yoyote ile, basi unakuwa uumbaji huo ni mzuri mkamilifu, unaolingana sawasawa katika kila njia, katika rangi yake, mwonekano wake, kuinuka juu kwake, na vilivyomo kama vile jua [na mwezi] na sayari zenye mwangaza. Vile visivyosonga miongoni mwake na vile vinavyosonga. Na pindi ukamilifu wake ulipokua jambo linalojulikana, Mwenyezi Mungu Mtukufu akatuamuru kuziangalia mara kwa mara na kutafakari katika pande zake. Akasema: "Hebu rudia kutazama!" Yaani, rudia kutazma kwa kuzingatia. "Je, unaona kosa lolote?"