انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الملك
السورة ٦٧

الملك

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٤

أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ ٱللَّطِيفُ ٱلْخَبِيرُ ١٤

{14} Kisha akasema akibainisha ushahidi wa kiakili juu ya elimu yake: "Asijue yule aliyeumba." Vipi asivijue yule aliyeumba viumbe, akavikamilisha sawasawa na akaviumba kuwa vizuri zaidi, vipi asivijue "naye ndiye Mjua siri, Mwenye habari?" Ambaye ujua wake na kuwa kwake na habari ya kila kitu kunafikia kila kitu, kiasi kwamba anafahamu vyema siri, dhamiri, vilivyofichikana na ghaibu zote. Na Yeye ndiye "anayejua siri na kilicho chini zaidi kuliko siri." Na katika maana za Al-Latwif (Mpole), ni kwamba Yeye ndiye mwenye kumfanyia upole mja wake na kipenzi chake, kwa hivyo unamfikishia wema na ukarimu kutokea pale asipotambua, na anamkinga mbali na uovu kutokea pale asipotarajia, na anampandisha daraja za juu kwa sababu ambazo hata mja mwenyewe hazijui, kiasi kwamba humwonjesha mambo anayochukia ili amfikishe kwenye mapenzi makubwa na mambo matukufu yanayotafutwa.