انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الملك
السورة ٦٧

الملك

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٢

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُم بِٱلْغَيْبِ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ كَبِيرٌ ١٢

{12} Alipotaja hali ya watu wa mashakani, walio waovu, akataja maelezo ya watu wema wenye furaha, akasema: "Hakika wale wanaomwogopa Mola wao Mlezi kwa ghaibu." Yaani, katika hali zao zote, hata katika hali ambayo hawezi akawaona isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee, hawamfanyii maasia, wala hawafanyi chini ya namna alivyowaamrisha. "Watapata maghfira" ya dhambi zao, na ikiwa Mwenyezi Mungu atawasamehe dhambi zao, atawalinda kutokana na uovu wake na atawalinda kutokana na adhabu ya Jahannamu "na wana ujira mkubwa." Na hayo ni yale aliyowaandalia Mwenyezi Mungu katika bustani za mbinguni ya neema ya kudumu, na ufalme mkubwa, na starehe zenye kuendelea kuwafikia, na makasri na majumba yaliyoinuka juu, na hurulaini wazuri, na wajakazi na watoto wadogo, na kubwa zaidi kuliko hilo ni radhi za Mwingi wa rehema ambazo atawapa wakazi wa bustani za mbinguni.